Norton Children’s inajitolea kutoa huduma za kiafya kwa wakaazi wageni zaidi wa Greater Louisville. Kwa wakimbizi wanaokuja Marekani, ambao wanastahiki kupokea ukaguzi wa kiafya, sisi hutoa huduma ya kiafya kamilifu kupitia programu yetu ya tathmini maalum ya watoto ya kiafya kwa wakimbizi katika Norton Children’s Medical Group – NuLu.
Norton Children’s Medical Group – NuLu ni ofisi ya daktari wa watoto inayokaribisha watoto wote, huku ikitia makini kundi za watu maalum, wakiwamo:
Hospitali yetu ina vifaa vya kutosha kuhudumia mahitaji tofauti ya kiafya ya mtoto, huku ikitoa huduma kama usimamizi wa uuguzi maalum, utegemezi wa afya ya kiakili, Progeamu ya Mfanyikazi wa Afya ya Jamii, wafanyikazi wa kijamii na huduma za kisaikolojia. Daktari wa meno wa watoto pia hupatikana kupitia ushirikiano wetu na University of Louisville School of Dentistry.
Watoto wakimbizi wanaofika Marekani wanaweza kupokea ukaguzi kamili wa kiafya unaojulikana kama tathmini ya kiafya ya mkimbizi katika Norton Children’s Medical Group – NuLu, huku ikifanywa kwa ushirikiano na wakala za eneo za wakimbizi kama Kentucky Refugee Ministries, Catholic Charities of Louisville na International Rescue Committee. Hakuna ada inayotozwa kwa mafamilia kwa miadi hii ya kiafya. Usafirishaji hufanywa na wakala, na huduma za ukalimani pia hutolewa. Tathmini hii hujumuisha:
Ingawa tathmini za afya ya wakimbizi kwa kawaida huratibiwa na wakala za kieneo za wakimbizi, aina ya wahamiaji wengine wapya kwa Marekani pia wanakaribishwa kupangia ukaguzi wa kiafya wa kwanza wa mtoto wao. Hakikisha unaleta rekodi zozote, kadi ya bima na historia ya chanjo kwa miadi yako ya kwanza.
Tunawahimiza familia ya wakimbizi ambao wamekamilisha tathmini zao za kiafya kufuatilia nasi kwa chanjo za kufikia, tathmini ya ukuaji na vipimo vya afya ya kiakili. Vipimo vya afya ya mtoto ya kila mwaka unapendekezwa kwa watoto wote. Panga miadi yako ya daktari wa meno na daktari wa kiafya katika siku sawa kwa urahisi.
Chanjo mpya ya COVID-19 inahitajika kwa mchakato wa kadi ya kijani (kadi ya mkaazi wa kudumu). Iwapo utachangua KUTOchukuwa chanjo hii au chanjo ya nyongeza (iwapo imefika muda wake), basi unatakiwa kujaza Fomu I-601, Ombi la Kusamehewa kwa Sababu za Kutokubaliwa, na uiwasilishe kwa wakili wako.
Watoto wakimbizi wanaostahiki huduma za mpasuaji raia wanaweza kupata usaidizi, ikiwamo kujaza Fomu I-698. Leta utambulisho wako uliyo na picha uliyopatiwa na serikali wakati wa kutia saini Fomu I-698. Iwapo umri wa mtoto ni wa miaka 14 au zaidi, basi ni lazima wahudhurie kutia saini fomu yao na pia ni lazima wawe na utambulisho wao wenyewe. Utapokea fomu zilizotiwa saini katika bahasha iliyofungwa utakayotuma pamoja na nyaraka zako zingine. Shauriana na wakala yako inayofaa na/au timu yako ya kisheria.
Ili kupanga miadi katika Norton Children’s Medical Group – NuLu, call (502) 588-8900, chaguo la 1. Kundi letu liko tayari kukusaidia na maswali ya kiafya na kukusaidia kupanga ziara yako.
Kwa rasilimali na taarifa kuhusu huduma za afya Marekani katika lugha zaidi ya Kiingereza, tembelea tovuti za mashirika yafuatayo. Tumekusanya orodha ya rasilimali za kitaifa na kieneo ili kutegemeza mahitaji ya kiafya ya familia katika Marekani.